Jumatano, 21 Desemba 2016




MATAIFA YOTE YATAKUSANYWA KATIKA HUKUMU

Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi. Mathayo 25:32.
Tukio la hukumu litawekwa ulimwengu wote ukiwepo; kwani katika hukumu hii serikali ya Mungu itathibitishwa na sheria yake itasimama ikiwa ni “takatifu, na ya haki, na njema.” Ndipo kila kesi itakapoamuliwa na hukumu itakapotolewa kwa wote. Ndipo Dhambi itakapoonekana kutovutia, bali itaonekana katika ukubwa wa ubaya wake wote.
“Na mataifa yote watakusanyika mbele zake.”… Kila tendo, dogo au kubwa, litatambuliwa. Kile ambacho hapa kimefikiriwa kuwa ni kidogo, wakati huo kitaonekana kama kilivyo. Senti mbili za mjane zitatambuliwa. Kikombe cha maji ya baridi kilichotolewa kwa ukarimu, gereza lililotembelewa, wenye njaa waliolishwa, -- kila tendo litaleta malipo yake. Na ule wajibu ambao haukutimizwa, lile tendo la ubinafsi, halitasahauliwa. Kwenye mahakama ya wazi mbele za kiti cha enzi cha Mungu, litatokea kwa namna tofauti kabisa ukilinganisha na lilivyoonekana wakati likitendwa… Itaonekana kwamba anasa hizi za kibinafsi na hali hii ya kukosa kiasi vimemfanya mwanadamu kuwa mpenzi wa anasa kuliko kumpenda Mungu… Lakini si lazima kwa yeyote kudanganywa; na wala hatutakuwa tumedanganywa kama tutakuwa tumekuwa na msimamo kikamilifu tukiwa pamoja na Kristo kumfuata yeye tupitapo kwenye taarifa mbaya au nzuri.
Tabia tunayoidhihirisha sasa, inaamua hali yetu ya wakati ujao. Furaha ya mbinguni itaonekana kwa kupatana na mapenzi ya Mungu na kama watu watakuwa washiriki wa familia ya kifalme ya mbinguni, itakuwa ni kwa sababu mbingu ilianza kuwa pamoja nao hapa duniani… Wenye haki watachukua kila sifa njema, kila uwezo wenye thamani, uliotakaswa, kwenye nyua za mbinguni na watachukua mbingu badala ya dunia. Mungu anajua nani walio raia watiifu kweli wa ufalme wake hapa duniani na wale watendao mapenzi yake hapa duniani kama yatendwavyo mbinguni, watafanywa kuwa wana familia ya kifalme ya mbinguni.


  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni