Jumanne, 23 Agosti 2016

TUNAUONEA FAHARI UFUFUO WA KRISTO

"Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele"
Yohana 11:25-26

Baada ya kusulubiwa kwa Kristo, makuhani na watawala hawakujisikia hisia ya ushindi ambayo waliitegemea. Hawakushangilia mafanikio yao Katika kunyamazisha Sauti ya Mwalimu Mkuu. Waliogopa.Tayari kifo chake kilivutia watu kuyatafakari maisha na tabia yake. Sasa Makuhani walisadiki kwamba walikuwa wameshindwa Katika majaribio yao ya kulipiza kisasi, hivyo sasa wakamwogopa zaidi kristo aliyekufa, zaidi sana, kuliko walivyomwogopa kristo aliyekuwa hai....

Nuru ya Mbinguni ililizunguka kaburi na Mbingu yote ikaangazwa kwa utukufu wa malaika. Malaika alilikaribia kaburi na baada ya kuliviringisha jiwe kana kwamba lilikuwa kokoto, aliketi juu yake. Kisha Sauti yake ikasikika, "Mwana wa Mungu, njoo huku nje; Baba yako anakuita"

Na Yesu akatoka kwenye kaburi kwa mwendo wa mshindi mkuu.kulikuwa na mlipuko wa ushindi, kwani familia ya Mbinguni ilikuwa inasubiri kumpokea; na yule malaika Mkuu, akifuatiwa na jeshi la Mbinguni, aliinama kwa heshima mbele zake Wakati Yeye, Mfalme wa Mbinguni, huku akiwa juu ya kaburi la Yusufu likilokuwa limepasuliwa, alitangaza, "Mimi ndimi huo ufufuo na uzima"

Viumbe wote walioumbwa wanaishi kutokana na mapenzi na nguvu ya Mungu. Wao Ni wapokeaji wa uzima wa Mwana wa Mungu. Hata wakiwa na uwezo na talanta kiasi gani, hata wakiwa na umahiri kiasi gani, huwa wanajazwa upya kwa uzima kutoka kwake aliye chanzo cha uzima wote. Yeye ni chemchemi, Chemchemi ya uzima .... Uzima ambao aliuweka chini Katika ubinadamu, aliutwaa tena na kuwapa binadamu. Alisema,
"Mimi nalikuja ili wawe na uzima, Kisha wawe nao tele"....
Kristio alikuja akawa mmoja pamoja na binadamu, ili ubinadamu upate kuwa Katika umoja na Roho na uzima pamoja naye. Kutokana kuwa na umoja huu Katika kutii Neno la Mungu, maisha yake yanakuwa maisha yao. Anamwambia aliyeungama, "Mimi ndiye huo ufufuo na uzima"
KRISTO ALISTAHIMILI MSALABA KWA AJILI YETU.

"tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba" Wafilipi 2:8
Image may contain: outdoor

Kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye milele ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Alikufa msalabani kama kafara kwa ajili ya Ulimwengu na kupitia kwa kafara yake ndipo baraka kuu inapokuja ambayo Mungu Anatupatia,--Karama ya Roho Mtakatifu. Baraka hii ni kwa ajili ya wote watakaompokea kristo.
Ulimwengu ulioanguka ni eneo la mapambano kwa ajili ya pambano kuu kabisa ambalo viumbe vyote vya Mbingu na vya duniani vimewahi kushuhudia. Sehemu hii iliteuliwa kama ukumbi wa maonesho ambapo pambano kuu kabisa lingepiganwa kati ya wema na uovu, Kati ya Mbingu na kuzimu.
Kila mwanadamu ana sehemu ya kufanya Katika pambano hili. Hakuna awezaye kusimama kwenye eneo huru. Ni lazima watu wamkubali au wamakatae Mwokozi wa ulimwengu. Wote, wawe kwa ajili ya Kristo au kinyume chake, ni mashahidi. Kristo anaita wale walio tayari kusimama chini ya bendela yake kuingia kwenye pambano pamoja naye kama askari waaminifu, ili wapate kurithi taji ya uzima. Wamefanywa kuwa wana na Binti za Mungu. Kristo amewaachia ahadi yake iliyo thabiti kwamba wale watakaokuwa washirika wa fedheha na mateso yake kwa ajili ya kweli Watapewa tuzo iliyo kuu kwenye ufalme wa Mbinguni.
Msalaba wa Kalvari umetoa changamoto na hatimaye utashinda nguvu zote za kidunia na za kuzimu. Msalabani, ndicho kiini cha mivuto yote na kutokea hapo Mivuto kusambaa. Hiki ni kivutio kikuu, kwani Katika huu Kristo alitoa uhai wake kwa ajili ya Watu. Kafara hii ilitolewa kwa kusudi la kumrejesha mwanadamu kwenye ukamilifu wake wa awali, naam na hata Zaidi. Ilitolewa ili kumpatia badiliko la tabia, kumfanya kuwa zaidi ya mshindi. Wale wanaomshinda adui mkuu wa Mungu na watu kwa nguvu ya Kristo, watachukua nafasi kwenye nyumba za mbinguni juu ya malaika ambao hawajawahi kuanguka dhambini.

Alhamisi, 11 Agosti 2016

UNAHESABIWA HAKI KWA DAMU YA KRISTO

"Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye"
Warumi 5:8-9
Kristo amefanya upatanisho kwa ajili ya dhambi, tena amebeba fedheha yake yote, dhihaka na adhabu; licha ya hivyo, huku akiibeba dhambi, ameleta haki ya milele, ili muumini apate kuwa bila waa mbele za Mungu....
Lakini wapo wengi wanaodai kuwa watoto wa Mungu ambao wamewekeza Katika kumtumainia sehemu zingine, badala ya kwenye damu ya Kristo pekee. Wanapoombwa sana kuweka imani yao kikamilifu kwa Kristo kama Mwokozi aliye kamili wengi wanadhihilisha ukweli kwamba wana imani Katika kile wanachofikiria kuwa wanaweza kufanya. Hawa husema, "ninayo mengi sana ya kufanya kabla sijafaa kuja kwa Kristo", mwingine husema," nitakapokuwa nimetenda kwa kadiri niwezavyo, yote niwezayo kutenda, ndipo Bwana Yesu atakapokuja kunisaidia". Wanafikiria kwamba wanayo kazi kubwa sana ya kufanya Wao wenyewe kuokoa roho zao na kwamba Yesu ataingia na kukifanyia Kazi kile kipande kinachopungua na kufanya kazi ya kumalizia kwa ajili ya wokovu wao. Maskini watu hawa, hawatakuwa na nguvu ndani yake Mungu hadi watakapomkubali Kristo kama Bwana na Mwokozi kamili. Hawawezi kuongeza chochote kwa ajili ya wokovu wao.
Wana wa Israel walitakiwa kunyunyizia miimo ya milango yao damu ya Mwana kondoo aliyechinjwa, ili Wakati malaika wa mauti akipita kwenye nchi, wapate kuepuka uangamivu. Lakini ikiwa badala ya kufanya kitendo hiki sahili cha imani na utii, wangezuia mlango na kuchukua tahadhari zote Katika kumzuilia mbali malaika mwangamizaji, taabu zao zingekuwa za bure ..... damu ilipoonekana kwenye miimo ya milango, ilitosha. Wokovu wa nyumba ulidhibitishwa.
Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya Wokovu, ni damu ya Yesu Kristo inayotutakasa kutoka katika dhambi zote. Kupitia ustahili wa damu yake, unaweza kushinda kila adui wa kiroho na kuponya kila udhaifu wa tabia.

Jumapili, 7 Agosti 2016

NAMSIFU M MWITA*** ***YESU ndiye mfalme

How The Sabbath Was Changed?

Pope Francis blames global economy, not Islam, for terrorism. What’s his solution?

Pope Francis blames global economy, not Islam, for terrorism. What’s his solution?
TUNASAFISHWA KWA DAMU YA YESU

"Damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote"

1 Yohana 1:7
Kuhusu Wakati wa Wayahudi, baadhi ya watu Wanasema kilikuwa kipindi ambacho hakikuwa na hali ya kuwepo kwa kristo, Hakikuwa rehema au neema. Kwa watu kama hao maneno ya Kristo aliyosema kwa Masadukayo yanawafaa, "hamyajui maandiko Wala uweza wa Mungu"
Wakati wa utamaduni wa kiyahudi ulikuwa ni Wakati wa udhihirisho wa ajabu wa uweza wa Mungu. Dhihirisho la kuwepo kwake lilikuwa la utukufu kiasi ambacho mwanadamu anayekufa asingeweza kustahimili. Musa, ambaye Mungu alimpenda sana alisema," nimeshikwa na hofu na kutetemeka "Lakini Mungu alimtia nguvu akaweza kustahimili utukufu huu wa ajabu na kufanya uso wa Musa kuakisi utukufu huu kutoka mlimani kiasi kwamba watu Hawakuweza kudumu kumtazama....
Mfano halisi wa kafara ulipangwa na Kristo, na Adamu akapewa kama kielelezo kinachoonesha Mwokozi anayekuja, ambaye angebeba dhambi za ulimwengu na kufa ili kuukomboa. Kupitia kwa Musa, Kristo alitoa maelekezo dhahiri kwa wana wa Israel kuhusu sadaka za kafara.....Ni wanyama wale tu waliokuwa Safi na wenye thamani, ambao wangemwakilisha Kristo kwa ubora zaidi, ndio waliokubalika kama sadaka kwa Mungu.....

Wana wa Israel walikatazwa Kula mafuta au damu ...sheria hii haikuhusu wanyama wa sadaka tu, bali pia ng'ombe wote waliotumika kwa chakula. Sheria hii ilikuwa imekusudiwa kusisitiza ndani yao ukweli wa muhimu kwamba kama isingekuwa dhambi, kusingekuwa na umwagaji wa damu ....
Damu ya Mwana wa Mungu iliwakilishwa na damu ya mnyama aliyechinjwa na Mungu alikuwa amewekeza dhana zilizo dhahiri na wazi zilizobainisha kati ya vitakatifu na vya kawaida. Damu ilikuwa takatifu, kwa namna ambavyo kupitia kumwagika kwa damu ya Mwana wa Mungu pekee ndiko kungeleta upatanisho kwa ajili ya dhambi.

Vilevile Damu ilitumika kusafishia hekalu kutokana na dhambi za watu, kwa namna hiyo kuonesha kielelezo cha damu ya Yesu Kristo ambayo ndio pekee iwezayo kutakasa tu toka Katika dhambi .

Alhamisi, 4 Agosti 2016

WOTE WANAOUTAZAMA MSALABA WATAISHI

    Hesabu 21:9
 "Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi"

     
      Bwana Yesu alikuwa amewalinda wana wa Israeli kutokana na Nyoka wenye sumu nyikani, Lakini hawajajua sehemu ya historia yao.
Malaika kutoka mbinguni walikuwa wameambatana nao na Katika nguzo ya wingu Wakati wa mchana na nguzo ya moto Wakati wa usiku, Kristo alikuwa mlinzi Wao Katika safari yao yote. Lakini wakawa na ubinafsi na kutoridhika na ili wasisahau uangalizi wake mkuu kwao, Bwana aliwapa fundisho chungu. Musa aliagizwa kuinua Nyoka wa shaba kwenye mti na kutangaza kwamba yeyeto ambaye angemtazama angeishi. Na wote waliomtazama waliishi. Walirejeshewa Afya mara moja.....
    
     Hiki kielelezo cha Yesu kufananishwa na Nyoka waliowauma kilikuwa cha ajabu sana. Ishara hii iliinuliwa kwenye mti na walikuwa waitazame wapate kupona. Hivyo Yesu alifanywa afanane na mwili wenye dhambi. Alikuja kama mbeba--dhambi....

      Ujumbe huohuo, unaoponya unasikika sasa. Unaelekeza kwa Mwokozi aliyeinuliwa kwenye mti ule wa aibu. Wale ambao wameumwa na yule Nyoka wa zamani, mwovu wanaagizwa kuangalia na kuishi.....wewe mwenyewe mtazame Yesu kama haki yako na kafara yako. Unapofanywa mwenye haki kwa imani, uchungu wa joka ambao unauma utaponywa.

      Bila msalaba ,Mtu asingeweza kuwa na umoja na Baba. Kila sehemu ya tumaini letu inategemea hapo. Kutokana na huo msalaba nuru ya upendo wa Mwokozi inang'aa, na wakati mwenye dhambi anapoinua macho yake kutoka chini ya msalaba akimtazama Yeye aliyekufa ili kumwokoa, anaweza kufurahia kwa shangwe yote, kwani dhambi zake zimesamehewa. Huku alipiga magoti msalabani, anakuwa amefikia sehemu ya juu kabisa ambayo Mtu anaweza kuifikia.
ASILI YETU
Mwanzo 1:1-8
-Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi-
Pamoja nchi ilikuwa utupu na giza lilitanda juu yake Roho ya Mungu ilitulia juu ya uso wa maji, ndipo Mungu akaanza kutamka iwe nuru, nayo nuru ikawepo
    -Mungu akaona nuru yakuwa ni njema na akatenga nuru na giza, Nuru mchana na giza Usiku. Pia siku hii Mungu alilitenga anga katikati ya maji akaliita anga Mbingu, ikawa asubuhi ikawa jion siku ya kwanza

 Fungu la 10. Mungu akapaita pale pakavu Nchi, makusanyiko ya maji akayaita Bahari. Mungu akaona kuwa ni vyema.
  -akasema na nnchi itoe majani , mche utoao mbegu kwa jinsi yake (yaani tofauti tofauti) na miche izaao matunda ambao mbegu zake zimo ndani yakekwa jinsi yake. Mungu akaona yakuwa ni vyema.

Fungu la 16. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa ule mkubwa utawale mchana na mdogo utawale usiku na akafanya na nyota pia.Mungu akaiweka katika anga la mbingu , itie nuru juu ya nchi. kutawala mchana na usiku kutenga nuru na giza.Mungu akaona ni vyema. ikawa asubuhi ikawa jioni siku nne (4)
  
Fungu la 20 na kuendelea inaelezea Uumbaji wa viumbe hai wa majini na ndege warukao juu ya anga wakiwepo na nyangumi  Mungu akavibariki na akasema Zaeni mkaongezeke mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi juu ya nchi.
-Ikawa jioni ikawa asubuhi siku ya tano(5).

Mungu akasema. Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa na nacho kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake.Mungu akaona ni vyema.

Fungu la 26: Mungu anasema na Tumfanye Mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, wanyama na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
-MUNGU AKAUMBA MTU KWA MFANO WAKE, KWA MFANO WA MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMUME NA MWANAMKE ALIWAUMBA.

Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi, nakuitiisha: mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Mwanzo 2:1.
Basi mbingu na nchi zikamalizika na jeshi lake lote.

Maelezo:
-Sisi ni wa thamani mno kwa Mungu wetu aliyetuumba kwa mikono yake mitukufu tofauti na wanyama, ndege na vyote tunavyoviona hapa duniani. Pia tuna wajibu ya kuvitunza vyote tulivyokabidhiwa na Muumbaji wetu.
-Ni wajibu wetu kuilinda miili yetu kwani ina thamani kubwa mmno na tumuombe Mungu atufundishe namna bora ya kuitunza miili yetu ili yesu atakaporudi mara ya pili aikute ikiwa misafi ifaayo kuingia katika mji aliyotuandalia.

MBALIKIWE WOTE KATIKA JINA LA YESU MWOKOZI WETU