TUNASAFISHWA KWA DAMU YA YESU
"Damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote"
1 Yohana 1:7
Kuhusu Wakati wa Wayahudi, baadhi ya watu Wanasema kilikuwa
kipindi ambacho hakikuwa na hali ya kuwepo kwa kristo, Hakikuwa rehema
au neema. Kwa watu kama hao maneno ya Kristo aliyosema kwa Masadukayo
yanawafaa, "hamyajui maandiko Wala uweza wa Mungu"
Wakati wa utamaduni wa kiyahudi ulikuwa ni Wakati wa udhihirisho wa ajabu wa uweza wa Mungu. Dhihirisho la kuwepo kwake lilikuwa la utukufu kiasi ambacho mwanadamu anayekufa asingeweza kustahimili. Musa, ambaye Mungu alimpenda sana alisema," nimeshikwa na hofu na kutetemeka "Lakini Mungu alimtia nguvu akaweza kustahimili utukufu huu wa ajabu na kufanya uso wa Musa kuakisi utukufu huu kutoka mlimani kiasi kwamba watu Hawakuweza kudumu kumtazama....
Mfano halisi wa kafara ulipangwa na Kristo, na Adamu akapewa kama kielelezo kinachoonesha Mwokozi anayekuja, ambaye angebeba dhambi za ulimwengu na kufa ili kuukomboa. Kupitia kwa Musa, Kristo alitoa maelekezo dhahiri kwa wana wa Israel kuhusu sadaka za kafara.....Ni wanyama wale tu waliokuwa Safi na wenye thamani, ambao wangemwakilisha Kristo kwa ubora zaidi, ndio waliokubalika kama sadaka kwa Mungu.....
Wana wa Israel walikatazwa Kula mafuta au damu ...sheria hii haikuhusu wanyama wa sadaka tu, bali pia ng'ombe wote waliotumika kwa chakula. Sheria hii ilikuwa imekusudiwa kusisitiza ndani yao ukweli wa muhimu kwamba kama isingekuwa dhambi, kusingekuwa na umwagaji wa damu ....
Damu ya Mwana wa Mungu iliwakilishwa na damu ya mnyama aliyechinjwa na Mungu alikuwa amewekeza dhana zilizo dhahiri na wazi zilizobainisha kati ya vitakatifu na vya kawaida. Damu ilikuwa takatifu, kwa namna ambavyo kupitia kumwagika kwa damu ya Mwana wa Mungu pekee ndiko kungeleta upatanisho kwa ajili ya dhambi.
Vilevile Damu ilitumika kusafishia hekalu kutokana na dhambi za watu, kwa namna hiyo kuonesha kielelezo cha damu ya Yesu Kristo ambayo ndio pekee iwezayo kutakasa tu toka Katika dhambi .

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni