UNAHESABIWA HAKI KWA DAMU YA KRISTO
Warumi 5:8-9
Kristo amefanya upatanisho kwa ajili ya dhambi, tena amebeba
fedheha yake yote, dhihaka na adhabu; licha ya hivyo, huku akiibeba
dhambi, ameleta haki ya milele, ili muumini apate kuwa bila waa mbele za
Mungu....
Lakini wapo wengi wanaodai kuwa watoto wa Mungu ambao wamewekeza Katika kumtumainia sehemu zingine, badala ya kwenye damu ya Kristo pekee. Wanapoombwa sana kuweka imani yao kikamilifu kwa Kristo kama Mwokozi aliye kamili wengi wanadhihilisha ukweli kwamba wana imani Katika kile wanachofikiria kuwa wanaweza kufanya. Hawa husema, "ninayo mengi sana ya kufanya kabla sijafaa kuja kwa Kristo", mwingine husema," nitakapokuwa nimetenda kwa kadiri niwezavyo, yote niwezayo kutenda, ndipo Bwana Yesu atakapokuja kunisaidia". Wanafikiria kwamba wanayo kazi kubwa sana ya kufanya Wao wenyewe kuokoa roho zao na kwamba Yesu ataingia na kukifanyia Kazi kile kipande kinachopungua na kufanya kazi ya kumalizia kwa ajili ya wokovu wao. Maskini watu hawa, hawatakuwa na nguvu ndani yake Mungu hadi watakapomkubali Kristo kama Bwana na Mwokozi kamili. Hawawezi kuongeza chochote kwa ajili ya wokovu wao.
Wana wa Israel walitakiwa kunyunyizia miimo ya milango yao damu ya Mwana kondoo aliyechinjwa, ili Wakati malaika wa mauti akipita kwenye nchi, wapate kuepuka uangamivu. Lakini ikiwa badala ya kufanya kitendo hiki sahili cha imani na utii, wangezuia mlango na kuchukua tahadhari zote Katika kumzuilia mbali malaika mwangamizaji, taabu zao zingekuwa za bure ..... damu ilipoonekana kwenye miimo ya milango, ilitosha. Wokovu wa nyumba ulidhibitishwa.
Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya Wokovu, ni damu ya Yesu Kristo inayotutakasa kutoka katika dhambi zote. Kupitia ustahili wa damu yake, unaweza kushinda kila adui wa kiroho na kuponya kila udhaifu wa tabia.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni