Alhamisi, 4 Agosti 2016

WOTE WANAOUTAZAMA MSALABA WATAISHI

    Hesabu 21:9
 "Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi"

     
      Bwana Yesu alikuwa amewalinda wana wa Israeli kutokana na Nyoka wenye sumu nyikani, Lakini hawajajua sehemu ya historia yao.
Malaika kutoka mbinguni walikuwa wameambatana nao na Katika nguzo ya wingu Wakati wa mchana na nguzo ya moto Wakati wa usiku, Kristo alikuwa mlinzi Wao Katika safari yao yote. Lakini wakawa na ubinafsi na kutoridhika na ili wasisahau uangalizi wake mkuu kwao, Bwana aliwapa fundisho chungu. Musa aliagizwa kuinua Nyoka wa shaba kwenye mti na kutangaza kwamba yeyeto ambaye angemtazama angeishi. Na wote waliomtazama waliishi. Walirejeshewa Afya mara moja.....
    
     Hiki kielelezo cha Yesu kufananishwa na Nyoka waliowauma kilikuwa cha ajabu sana. Ishara hii iliinuliwa kwenye mti na walikuwa waitazame wapate kupona. Hivyo Yesu alifanywa afanane na mwili wenye dhambi. Alikuja kama mbeba--dhambi....

      Ujumbe huohuo, unaoponya unasikika sasa. Unaelekeza kwa Mwokozi aliyeinuliwa kwenye mti ule wa aibu. Wale ambao wameumwa na yule Nyoka wa zamani, mwovu wanaagizwa kuangalia na kuishi.....wewe mwenyewe mtazame Yesu kama haki yako na kafara yako. Unapofanywa mwenye haki kwa imani, uchungu wa joka ambao unauma utaponywa.

      Bila msalaba ,Mtu asingeweza kuwa na umoja na Baba. Kila sehemu ya tumaini letu inategemea hapo. Kutokana na huo msalaba nuru ya upendo wa Mwokozi inang'aa, na wakati mwenye dhambi anapoinua macho yake kutoka chini ya msalaba akimtazama Yeye aliyekufa ili kumwokoa, anaweza kufurahia kwa shangwe yote, kwani dhambi zake zimesamehewa. Huku alipiga magoti msalabani, anakuwa amefikia sehemu ya juu kabisa ambayo Mtu anaweza kuifikia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni