Jumanne, 23 Agosti 2016

KRISTO ALISTAHIMILI MSALABA KWA AJILI YETU.

"tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba" Wafilipi 2:8
Image may contain: outdoor

Kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye milele ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Alikufa msalabani kama kafara kwa ajili ya Ulimwengu na kupitia kwa kafara yake ndipo baraka kuu inapokuja ambayo Mungu Anatupatia,--Karama ya Roho Mtakatifu. Baraka hii ni kwa ajili ya wote watakaompokea kristo.
Ulimwengu ulioanguka ni eneo la mapambano kwa ajili ya pambano kuu kabisa ambalo viumbe vyote vya Mbingu na vya duniani vimewahi kushuhudia. Sehemu hii iliteuliwa kama ukumbi wa maonesho ambapo pambano kuu kabisa lingepiganwa kati ya wema na uovu, Kati ya Mbingu na kuzimu.
Kila mwanadamu ana sehemu ya kufanya Katika pambano hili. Hakuna awezaye kusimama kwenye eneo huru. Ni lazima watu wamkubali au wamakatae Mwokozi wa ulimwengu. Wote, wawe kwa ajili ya Kristo au kinyume chake, ni mashahidi. Kristo anaita wale walio tayari kusimama chini ya bendela yake kuingia kwenye pambano pamoja naye kama askari waaminifu, ili wapate kurithi taji ya uzima. Wamefanywa kuwa wana na Binti za Mungu. Kristo amewaachia ahadi yake iliyo thabiti kwamba wale watakaokuwa washirika wa fedheha na mateso yake kwa ajili ya kweli Watapewa tuzo iliyo kuu kwenye ufalme wa Mbinguni.
Msalaba wa Kalvari umetoa changamoto na hatimaye utashinda nguvu zote za kidunia na za kuzimu. Msalabani, ndicho kiini cha mivuto yote na kutokea hapo Mivuto kusambaa. Hiki ni kivutio kikuu, kwani Katika huu Kristo alitoa uhai wake kwa ajili ya Watu. Kafara hii ilitolewa kwa kusudi la kumrejesha mwanadamu kwenye ukamilifu wake wa awali, naam na hata Zaidi. Ilitolewa ili kumpatia badiliko la tabia, kumfanya kuwa zaidi ya mshindi. Wale wanaomshinda adui mkuu wa Mungu na watu kwa nguvu ya Kristo, watachukua nafasi kwenye nyumba za mbinguni juu ya malaika ambao hawajawahi kuanguka dhambini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni